Nafasi Ya Matangazo

December 31, 2013

Majina ya wanafunzi wa darasa la saba 2013 ambao wamefaulu na kuchaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari (kidato cha kwanza) mwaka 2014 yanapatikana katika mbao za matangazo katika shule za Msingi walizo soma watoto hao na katika ubao wa m,atangazo wa ofisi za Kata zilizo jirani. 

Hivyo wazazi na  wanafunzi wametakiwa kufika katika shule husika au katika Ofisi za Kata kuangalia majina ya wanafunzi hao na shule walizo chaguliwa. Pichani ni Baadhi uya wanafunzi na wazazi wakiangalia majina hayo katika ofisi ya Mtendaji Kata ya Makurumla jijini Dar es Salaam jana.
Posted by MROKI On Tuesday, December 31, 2013 5 comments

5 comments:

  1. Matokeo ya masomo ya drs vii yalirushwa mtandaoni jambo ambalo ni zuri linalokwenda na wakati. Majina ya kwenda sekondari nini kimejili hata yasirushwe ? Au BRN ilikuwa ni nguvu za soda ?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hujui kwamba kuprint na kubandika ubaoni watu wanapewa ruzuku? Hizi zinaitwa fursa mkuu

      Delete
  2. Serikali isiyomakini siku zote ina nguvu za soda

    ReplyDelete
  3. umevulugwa wewe mbona matokeo yenyewe hatuyaoni hapa,yan wiz mtupu........

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo