Nafasi Ya Matangazo

April 17, 2014

Kutoka kushoto: Wasanii Dk. Cheni, Bi. Mwenda, Profesa Jay na Wema Sepetu wakishiriki kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa GlobaL TV Online jana.
Wema Sepetu na Profesa Jay wakifunua vitambaa wakati wa uzinduzi wa GlobaL TV Online jana katika ofisi za Global Publishers Ltd.
GlobaL TV Online baada ya kuzinduliwa rasmi.
Mkurugenzi wa Global Publishers & General Enterprises Ltd, Eric Shigongo pamoja na staa wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu wakikata keki wakati wa uzinduzi huo.
Mkongwe wa sanaa ya maigizo Bongo, Fatuma Makongoro 'Bi. Mwenda' akijiandaa kufungua shampeini.
Shampeini zikiwa tayari kufunguliwa.
Waalikwa na wafanyakazi wa Global wakigonga 'Cheers'.
Prof Jay, Bi. Mwenda na Steve Nyerere  wakigonga 'cheers'.
Shigongo akigonga 'cheers' na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Richard Manyota (kulia) na Oscar Ndauka ambaye ni Mhariri Kiongozi Magazeti Pendwa (katikati).
Mastaa wakigonga cheers.
...Cheers. Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, wachapishaji wa Magazeti ya Uwazi, Championi, Amani, Risasi, Ijumaa na Ijumaa Wikienda jana ilizindua Global TV Online ambayo ni televisheni inayoruka mtandaoni kupitia tovuti ya kampuni hiyo ya www.globalpublishers.info ndani ya ofisi zake zilizopo Mwenge-Bamaga jijini Dar es Salaam. Katika uzinduzi huo, mastaa kibao walihudhuria na kupata fursa ya kuona baadhi ya vipindi kutoka Global TV Online pamoja na kutoa maoni yao kuhusu uboreshwaji wa TV hiyo. Mbali na tukio hilo, mastaa waliongoza zoezi la kukata utepe, kufungua shampeini na kukata keki kuashiria uzinduzi rasmi wa Global TV Online.
Posted by MROKI On Thursday, April 17, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo